Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amehitimisha ziara yake ya kikazi ya siku nne mkoani Tabora ambapo amehitimisha ziara hiyo kwa kuongea na viongozi pamoja na watimishi wa mkoa huo katika majumuisho ya ziara yake.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiongea na viongozi pamoja na watumishi wa Mkoa wa Tabora leo August 13, 2017 wakati wa majumuisho ya ziara yake Mkoa wa Tabora. Ambo ume fanyika katika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiagana na Mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Agrey Mwandi katika Uwanja wa Ndege wa Tabora leo August 13, 2017 baada ya kumaliza ziara ya siku Nne katika Mkoa wa Tabora, katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Queen Mwashinga
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa .akiwapungia Mkono wa kwaheri Viongozi pamoja na wananchi wa Mkoa wa Tabora ambao walifika kumuaga katika Uwanja wa Ndege wa Tabora baada yakumaliza ziara ya siku Nne ya kikazi katika Mkoa wa Tabora leo August 13,2017