Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, jana alimtembelea na kumpa pole waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye aliyelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Waziri Mkuu aliambata na mkewe, Mama Mary Majaliwa ambapo walikutana pia na mke wa Sumaye, Mama Esther Sumaye na kuzungumza.

Majaliwa, Sumaye, Mama Majaliwa na mama Sumaye

Sumaye amelazwa katika hospitali hiyo kwa takribani siku tano zilizopita akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo.

Juzi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli alimtembelea Waziri Mkuu huyo mstaafu ambapo madaktari walimhakikishia kuwa hali yake inaimarika.

 

 

 

 

Njonjo Amaliza Tetesi Ajiunga Na Newcastle Utd
Picha ya Ronaldo akimshika mchumba wa Messi yazua gumzo, 'Messi hakupenda'