Rapa Tyga amemvuruga tena mrembo wake Kylie Jenner ikiwa ni siku chache tangu akumbwe na skendo ya kumshawishi binti wa miaka 14 kupitia Instagram kuwa mpenzi wake.

US Weekly limeripoti kuwa Tyga amebainika kuwa alichepuka na mwanamitindo mrembo wa Brazil aliyetajwa kwa jina la Annalu Cardoso.

Tyga na Carodoso walikutana katika zoezi la kushuti moja kati ya video zake ambapo uzuri wa mrembo huyo ulimzidia rapa huyo akaamua ‘kujilipua’.

@ohrangutang @cristinapilo

A photo posted by Annalu (@annaluyzacardoso) on

Chanzo kimeiambia US Weekly kuwa rapa huyo alianza kuchat na mrembo huyo ambaye ni mwanamitindo na ghafla uhusiano wao ukaenda kwenye hatua ya pili.

Van Gaal Agusia Jambo Dhidi Ya Pep Guardiola
Wastara afunga ndoa na Mbunge