Mwanasiasa machachari wa Kenya, Miguna Miguna amelazwa hospitalini Dubai siku moja baada ya kuondolewa kwa nguvu nchini Kenya na ndege ya shirika la Emirates.
Picha za ‘selfie’ zilizowekwa kwenye akaunti ya Twitter ya Odeo Sirari na kuripotiwa pia na BBC zimemuonesha Miguna akiwa amelala kitandani katika hospitali moja, lakini kukuwa na maelezo zaidi.
Miguna Miguna’s hospital bed selfies from Dubai pic.twitter.com/uacJD57Eq8
— Odeo Sirari (@OdeoSirari) March 29, 2018
Juzi, Miguna alipambana na maafisa wa usalama wa Serikali ya Kenya waliomzuia kuingia nchini humo akitokea nchini Canada alikopelekwa kwa nguvu awali kwa madai ya kuwa alikana uraia wa Kenya.
Mwanasheria huyo alisafirishwa tena jana baada ya zoezi la awali la kumsafirisha juzi kushindikana nakuendelea kushikiliwa katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta.
Mvutano kati ya Miguna na Serikali iliwaibua viongozi wa ngazi za juu wa upinzani akiwemo Raila Odinga aliyefika katika uwanja huo wa ndege.
Hata hivyo, juhudi za Odinga aliyekuwa anajaribu kupiga simu hazikuzaa matunda.
Miguna alifukuzwa Kenya saa chache baada ya kukamatwakwa kwa kosa la kushiriki zoezi la kumuapisha Odinga kuwa ‘Rais wa Watu’, na kujitangaza kuwa kiongozi wa vuguvugu la National Resistance Movement (NRM).