Olivia Jordan, jana usiku alitimiza sehemu kubwa ya ndoto ya maisha yake baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa taji la mrembo wa Marekani (Miss USA 2015) akiwafunika warembo 50 walioshindania taji hilo.

Pamoja na mambo mengine, ushindi wa Olivia mwenye umri wa miaka 26, ulitokana na upeo mkubwa wa kujibu maswali na kujieleza. Aliwashawishi zaidi majaji alipoelezea suala la ubaguzi wa rangi ambalo limekuwa tatizo katika nchi hiyo iliyoshuhudia mauaji yanayotokana na ubaguzi.

“We still need to talk about race relations,” alisema. “We really need to work on being an accepting society. No matter your race, no matter your gender. Everyone needs to be given the same rights and opportunities.”

Olivia Jordan ambaye pia ni muigizaji, alishiriki shindano hilo kama mrembo aliyeiwakilisha Oklahoma.

Lowassa kuhamia Ukawa? Viongozi Wa Chadema ‘wanena’
Roger Federer Ailaumu Mvua