Jumba la sanaa huko Miami Beach, Florida Marekani Ijumaa iliyopita liligeuka kuwa eneo la tukio baya la kweli baada ya mwanamke mmoja kumchoma kisu mara mbili mwanamke mwengine huku watu wakidhani ni sehemu ya maigizo.

Kwa mujibu wa mtandao wa Miamiherlad, mwanamke huyo alimchoma mwenzake kisu kwenye mkono na shingoni baada ya kuzuka ugomvi kati yao.

Stabbing 2

Msemaji wa polisi wa Miami Beach, Det. Kathleen Prieto, alisema kuwa majeraha ya mhanga wa tukio hilo hayakusababisha tishio kubwa la maisha na kwamba alikimbizwa hospitali ambapo anapata matibabu.

Stabbing3

Baadhi ya mashuhuda waliuambia mtandao wa Miamiherald kuwa walipoliona tukio hilo waliamini ilikuwa sehemu ya maonesho tu lakini baadae walishtuka kuona damu halisi.

Magufuli aitumbua Bandari, Amsimamisha Katibu Mkuu, Avunja Bodi na Kutimua maafisa
Mawaziri Wa JK Watajwa majina ya Mawaziri wa Magufuli yaliyovuja