Msimu mpya wa mwaka 2016 wa Kipindi cha The Playlist cha 100.5 Times Fm kilizinduliwa kwa kishindo Jumamosi iliyopita (January 9) na kuambatana na hafla fupi iliyohusisha ‘mastaa’ kadhaa.

Hafla hiyo ilifanyika sambamba na urushaji wa matangazo moja kwa moja katika kipindi hicho ambacho awali kilikuwa kinaruka kuanzia saa 10 kamili jioni hadi saa 12 jioni, na sasa kimehamishiwa Jumamosi kuanzia saa 6 kamili hadi saa 8 mchana.

Mtangazaji wa imes Sandra akikata keki

Mtangazaji wa imes Sandra akikata keki

Mwaka 2015 ulikuwa mwaka wa mafanikio makubwa kwa kipindi cha The Playlist cha 100.5 Times Fm kwa mujibu wa ‘Brand Manager’ wa kipindi hicho, Omary ‘Lil Ommy’ Tambwe.

G Nako akifungua Champagne

G Nako akifungua Champagne

Lil Ommy ameiambia Dar24 kuwa pamoja na kuwa na mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya wasikilizaji na kuanza kutoa jarida la kipindi hicho la The Playlist, walikusanya maoni ya wasikilizaji na wadau na kuyafanyia kazi katika msimu mpya wa mwaka 2016 uliozinduliwa kwa kishindo.

Lil Ommy (Katikati) akiwa na baadhi ya wasanii waliohudhuria uzinduzi

Lil Ommy (Katikati) akiwa na baadhi ya wasanii waliohudhuria uzinduzi

“Mwaka huu The Playlist imeshiba zaidi. Wasikilizaji watapata zaidi ya wanachotegemea. Ubunifu wa kutosha, exclusive interviews zenye maswali ya kibabe pamoja nyimbo na movies zilizobamba. Habari zote kubwa za burudani bila kusahau fashion za kijanja zinazokiki,” alisema Lil Ommy na kuwashukuru wasikilizaji na wadau wote waliokiwezesha kipindi hicho mwaka uliopita.

The Playlist huwaalika mastaa studio na kuchagua nyimbo wanazozipenda pamoja na kujibu maswali mbalimbali.

Billnas na Chemical wakihojiwa

Billnas na Chemical wakihojiwa

Mhariri wa Bongo5, Fredrick Bundala akibadilishana mawazo na Joh Makini

Mhariri wa Bongo5, Fredrick Bundala akibadilishana mawazo na Joh Makini

Lil Ommy hewaniben Pol ndani ya The PlaylistThe Playlist 2Harmonizor

David Luiz Amuita Kijanja Diego Costa
Afisa Elimu ampiga makofi mwalimu kwa uchelewaji