Kila mwaka huwa una matukio yake makubwa yanayoacha alama katika mwaka huo na hata kuendelezwa katika mwaka unaofuata. Mwaka 2015 ulikuwa na mengi lakini moja kati ya mitindo iliyopata  umaarufu mkubwa na kuwa wa kipekee duniani ni mtindo wa ‘kuotesha’ mmea katikati ya utosi ulioshika kasi nchini China.

Kwa kuangalia unaweza kufikiri ni kweli wachina walikuwa wameotesha mmea katikati ya utosi, hali iliyowafanya mataifa mengine yauangalie kwa jicho la tatu mtindo huu ulioshika kasi nchini humo kama mtindo wa unyoaji wa kuweka ‘njia aka ‘Way’ pembeni kidogo ya kichwa ulivyoshika kasi miaka ya 1990’s nchini Marekani na mataifa mengine.

Lakini kiuhalisia, wachina hao walikuwa wakiweka mmea feki wa plastic (bondo), mmea uliokuwa maarufu na unaopendwa unaotengeneza virutubisho vya nywele na kuacha nywele zikiwa na hali nzuri ya unyevu (Sprout) .

MMEA 3

Mtindo huu ulianza kuonekana mapema mwezi Septemba 2015 lakini hakuna anayefahamu nani aliyeuanzisha, japo ulianza kushamiri kwanza katika eneo la Chengdu. Wanaume, wanawake na watoto walitumia takribani dola moja ya kimarekani ($1) kupata mtindo huo.

Mmmoja kati ya wauzaji aliiambiaa CNN kuwa alikuwa akiuza wastani wa mimea feki hiyo 200 kila baada ya saa tatu.

 

Wanaoumaliza Mwaka na Baraka za Uteuzi wa Magufuli Hawa Hapa
Serikali Kushusha rungu kwa redio na TV zitakazocheza Muziki wa Nje Kuliko wa Nyumbani