Kocha Mpya wa Klabu ya AFC Leopards ya Kenya Patrick Aussems rasmi ameanza ya kukinoa kikosi cha klab hiyo tayari kwa michezo ya Ligi Kuu Nchini Kenya.
Aussems ambaye bado anakumbukwa na wadau wa soka la Bongo kufuatia mazuri alioyafanya akiwa na Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba SC, ameanza majukumu yake AFC Leopards siku moja baada ya kutambulishwa kama kocha mkuu.
Jana jioni kocha huyo kutoka nchini Ubelgiji aliwasili katika uwanja wa mazoezi wa AFC Leopards akiwa na viongozi wa klabu hiyo, na kwa mara ya kwanza alikutanishwa na wachezaji wake na kuanza kazi rasmi.
Aussems aliwasili nchini Kenya Jumamosi na kutazama mchezo wa derby dhidi ya Gor Mahia kwenye Uwanja wa Kasarani Siku ya Jumapili, amechukua nafasi ya Tomas Trucha ambaye aliachia majukumu yake klabuni hapo
AFC Leopards ilikua haina kocha tangu Trucha ajiuzulu, akidai viongozi wengine walikuwa wakiingilia kazi yake.
Raia huyo wa Jamhuri ya Czech aliteuliwa kuwanoa mabingw ahao wa Kenya 13 mwanzoni mwa Novemba, kwa lengo la kuisaidia timu kutoa changamoto kwenye Mshike Mshie wa Ligi Kuu ya Kenya msimu huu 2020/21.