Serikali imetoa picha rasmi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli ambayo imeanza kuuzwa leo (Januari 8) katika ofisi za Idara ya Habari Maelezo katika mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam pamoja na Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA).

Picha hiyo itauzwa kwa shilingi elfu kumi na tano tu bila kuwa na frame. Kadhalika, picha ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere itauzwa kwa shilingi elfu tano tu.

Picha hizo zinapaswa kuwekwa kwenye ofisi zote za serikali, ofisi za mashirika ya umma na ofisi za mashirika na ofisi binafsi.

Aidha, serikali imetoa onyo kwa wale wanaosambaza picha isiyo rasmi. Imewakumbusha watanzania kuwa mwenye haki miliki ya picha hiyo ni Idara ya Habari Maelezo.

Mtuhumiwa namba Moja Kesi Ya Mauaji ya Dk. Mvungi Afariki
Kilichomkuta Aliyevaa Bomu Feki la Kujitoa Mhanga jijini Paris