Kikosi cha Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, kimewasili mjini Khartoum, Sudan usiku wa kuamkia leo, tayari kwa mchezo wa mzunguuko wa tatu wa Ligi ya Mabingwa hatua ya Makundi.
Simba SC iliwasili mjini humo ikitokea Addis Ababa, Ethiopia ilipobadilisha ndege, baada ya kuondoka jijini Dar es salaam, majira ya jana jioni.
Leo Alhamis kikosi cha Simba SC kitaanza mazoezi kikiwa mjini Khartoum, na kitafanya hivyo kesho kwenye uwanja Al Merrikh utakaotumika keshokutwa Jumamosi (Machi 06).
Wachezaji wa Simba SC waliosafiri na kuwasili salama mjini Khartoum ni Aishi Manula, Beno Kakolanya, Ally Salim, Shomari Kapombe, Joash Onyango, Pascal Wawa, Erasto Nyoni, Gadiel Michael, Mohamed Hussein, Jonas Mkude, Rarry Bwalya na Mzamiru Yassin.
Luis Miquissone, Hassan Dilunga, Ibrahim Ajibu, Clatous Chama, Francis Kahata, Meddie Kagere, John Bocco, Miraji Athuman, Kope Mugalu, Peter Muduhwa, Tadeo Lwanga, Kenedy Juma na David Kameta.
Simba SC inaongo za msimamo wa ‘KUNDI A’ kwa kumiliki alama sita, baada ya kuzifunga AS Vita Club ya DR Congo na Al Ahly ya MIsri.