Picha: Spika Ndugai na viongozi wengine walivyofika nyumbani kwa Mkapa
5 years ago
Spika wa Bunge, Job Ndugai ameambatana na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Zubeir Ali Maulid pamoja na Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai wamefika nyumbani kwa Rais wa Awamu ya Tatu, Hayati Benjamin William Mkapa kutoa pole kwa mjane Mama Anna Mkapa Masaki, Jijini Dar es Salaam.
Katika hatua nyingine, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya TPB, Sabasaba Moshingi (katikati), amefika nyumbani kwa hayati, Benjamin Mkapa Rais Mstaafu awamu ya tatu kutoa pole kwa Mama Anna Mkapa, nyumbani kwao Mtaa wa Masaki jijini Dar es Salaam.