Wanawake wanaotumikia vifungo mbalimbali katika moja kati ya magereza hatari la ‘Talavera Bruce lililoko Rio de Janeiro nchini Brazil wameshiriki katika shindano la kumsaka mrembo wa gereza hilo.

Miss Criminal 2015

Shindano hilo lililoendeshwa kwa mbwembwe likiwa na jina la ‘Miss Criminal 2015’ lilipelekea mfungwa aliyetajwa kwa jina la Michelle Neri Rangel mwenye umri wa miaka 27 kuibuka mshindi.

Miss Criminal 2015 part 2

Rangel alihukumiwa kifungo cha miaka 39 jela kwa kosa la kufanya ujambazi wa kutumia silaha ikiwa ni pamoja na nyongeza ya kifungo cha miaka 6 jela kwa kufanya biashara ya kuuza mwili ndani ya gereza hilo.

Mshindi, Miss Criminal 2015

Washiriki wa shindano hilo walipambwa na kuvalishwa magauni mazuri na kupita kwa mwendo wa paka mbele ya majaji.

 

Burna boy Aponda Tuzo Za Nigeria, Adai Zimejaa Siasa
Zitto Kabwe Adai Lowassa Aliwavuruga