Wakati pazia la uchukuaji fomu za kugombea nafasi za Ubunge, Uwakilishi na Udiwani likifunguliwa, baadhi ya wanasiasa maarufu wamekuwa mstari wa mbele kuchukua fomu hizo wakiwepo mawaziri.
Mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Fredrick Lowassa amechua fomu ya kuomba ridhaa ya chama cha mapinduzi (CCM) ya kugombea ubunge jimbo la Momnduli.
Waziri wa Uwekezaji, Angela Kairuki amechukua fomu ya kugombea Ubunge jimbo la Same Magharibi.
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima achukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambalo lilikuwa chini ya Halima Mdee wa CHADEMA.
Dkt. Tulia Ackson amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea ubunge Jimbo la Mbeya Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mrisho Gambo achukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea ubunge Jimbo la Arusha Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Wengine waliochukua ni Mlinzi wa zamani wa Baba wa Taifa, Aloyce Tendewa ambaye amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea ubunge Jimbo la Kilombero, Francis Nanai, Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa na Chama cha Mapinduzi kuwa mgombea ubunge katika Jimbo la Kawe.