Wananchi waliokuwa wanaishi katika eneo la bonde la Mkwajuni jijini Dar es Salaam wamepinga hatua za kubomolewa nyumba zao na kufanya vurugu iliyoambatana kufunga barabara kuu katika eneo hilo.

Shuhuda wa tukio hilo ameiambia Clouds Fm kuwa wananchi hao walipinga zoezi la kubomolewa nyumba zao leo na kuwafanyia fujo askari wawili waliokuwa wameambana watu waliokuwa wanaweka alama za X.

mkwajuni2

“Waliwakimbiza wale askari wawili na waweka X na baadae wakaanza kuchoma matairi na kufunga barabara,” alisema shuhuda huyo.

mkwajuni3

Hata hivyo, jeshi la polisi lilifika katika eneo hilo na kurudisha hali ya utulivu huku magari ya zima moto yakizima moto wa matairi na kuyaondoa barabarani. Hali imerejea kuwa shwari katika eneo hilo.

mkwajuni4

Rais Wa Soka Barani Asia Atua Tanzania
Ripoti: Asilimia 1 ya matajiri wanamiliki utajiri zaidi ya mali za watu wote duniani