Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini kati, Askofu Dkt. Solomoni Massangwa akimkabidhi fimbo Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu kama ishara ya Mchungaji mwema aliyetoa maisha yake kwa ajili ya kondoo, wakati wa tukio la kuwekwa wakfu na kusimikwa kazini kwa Askofu huyo, Lushoto Mkoani Tanga, Mei 9, 2021.
Askofu wa Dayosisi ya Mashariki ya Ziwa Victoria Mwanza, Askofu Andrew Gule akimvisha kofia Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu kama alama ya kazi ya ukuhani unavyokabidhiwa katika kanisa la Mungu, wakati wa tukio la kuwekwa wakfu na kusimikwa kazini kwa Askofu Dkt. Msafiri, Lushoto Mkoani Tanga, Mei 9, 2021.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT), baada ya tukio la kusimikwa kwa Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu kuwa Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Lushoto Mkoani Tanga, Mei 9, 2021.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu baada ya kusimikwa kuwa Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, kushoto ni mke wa Askofu huyo Marry Msafiri Mbilu, Lushoto Mkoani Tanga, Mei 9, 2021.
Serikali yatangaza nafasi za ajira
Serikali yamkabidhi Kikwete nyumba ya kuishi