Viazi ni chakula bora. Lakini muonekano wa kiazi asilia kutoka ardhini huchukuliwa kama kina muonekano usiovutia sana.

Huenda ndio sababu wengi huonekana kwenye mitandao wakiweka picha za vyakula vinavyovutia sana lakini sio picha ya kiazi cha asili ambacho hata hakijamenywa. Lakini mtu mmoja nchini Uingereza yeye ameona picha tu ya kiazi hicho ni dhahabu kwake na ametoa zaidi ya bilioni mbili kuhakikisha anainunua picha hiyo.

Mpiga picha Kevin Abosch aliliambia jarida la The Sunday Times kuwa alikuwa akinywa mvinyo na tajiri huyo ambaye alikuwa akitolea macho picha ya kiazi iliyokuwa imewekwa ukutani.

”Tulikuwa tumekunywa glasi mbili za mvinyo, nilifurahi sana. Lakini baada ya glasi zingine mbili za mvinyo bwana huyo alinisisitizia kuwa , ‘kwa kweli naipenda sana picha hiyo sijui iwapo unaweza kuniuzia hiyo”, mpiga picha huyo alisimulia.

Picha hiyo iliambana na mboga nyingine asilia.

Alisema kuwa walikubaliana bei ya $1066199.97 na baadae kila mmoja akashika njia yake. Lakini baada ya wiki mbili, tajiri huyo alikamilisha malipo hayo na kupokea picha yake ya kiazi ambayo mpiga picha huyo aliipiga mwaka 2010 katika mojawapo ya misururu ya viazi asilia.

Mpiga picha huyo huuza picha zake bei aghali siku zote, kati ya dola 285. Alipata umaarufu kwa kuwapiga picha waigizaji maarufu kama Johnny Depp na muigizaji na mtayarishaji nyota Steven Spielberg.

Nape: TBC haitarusha 'Live' Bunge kuanzia Leo ili Kubana Matumizi
Takukuru kutumbua majipu 36, Lake Oil yanaswa kukwepa kodi ya Mabilioni