Picha iliyochukuliwa hivi karibuni katika hafla ya utoaji tuzo ya Ballon d’Or ya mwaka 2015 ikimuonesha Cristiano Ronaldo akiwa amemshika mkono na kumkazia macho mchumba wa Lionel Messi, Antonella Roccuzzo, huku Messi na Neymar wakiangalia imezua jambo.

Wataalam wa saikolojia wameichambua picha hiyo na kuitolea maelezo yanayoonesha kuwa Messi alikuwa hajisikii vizuri (uncomfortable) wakati anashuhudia tukio hilo.

Ushahidi juu hilo, inaelezwa kuwa ni namna ambavyo ameonekana akikuna sikio lake huku akiachia tabasamu ‘feki’.

Wanasaikolojia hao wamemmulika Neymar aliyekuwa anaangalia pia na kumuwekea maneno, “I swear to God, if you so much as look at my boy’s lady again..!”

Picha ina tabia ya kuongea lugha ambayo kila mmoja anaweza kuitafsiri kadri awezavyo bila kujali mipaka. Huenda wewe pia ukawa umepata tafsri yako juu ya picha hii inayoongea mengi.

Picha: Majaliwa Amtembelea Sumaye Hospitalini
Staa wa 'Teen Wolf' ajilipua na hili