Mchoro wa picha ya Yesu unaojulikana kama Salvator Mundi (Mkombozi wa Dunia) wa miaka 500 iliyopita unaodhaniwa kuchorwa na Leonardo da Vinci, umeuzwa jijini New York kwa kiasi cha dola milioni 450.

Leonardo da Vinci alifarika dunia mwaka 1519 na kuacha michoro zaidi ya 20 iliyobaki, na huo ni mmoja wapo wa michoro ambao unaaminika kuchorwa mwaka 1505 hivyo kuwa miongoni mwa picha ghari duniani.

Aidha, picha hiyo inamuonyesh Yesu akiwa ameinua mkono mmoja huku mwingine ukishika kioo, kitu ambacho kimekuwa ni kivutio kwa watu mbalimbali.

Mwaka 1958 mchoro huo uliuzwa kwenye soko la mnada jijini London kwa Dola 60. wakati huo mchoro huo uliaminiwa kuwa kazi ya mfuasi wa Leonardo na wala haukuwa wa Leonardo mwenyewe.

Hata hivyo, miaka minne iliyopita mchoro wa picha hiyo ulinunuliwa na raia wa Urusi kwa dola milion 127.5 lakini wakati huo haukuuzwa katika mnada.

Kigogo wa Takukuru apandishwa kizimbani
Fellaini awaweka njia panda viongozi wa Man Utd