Kikosi cha Young Africans kimewasili salama Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam, kikitokea jijini Dodoma.

Young Africans jana Jumapili (Julai 18) ilicheza mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu msimu wa 2020-21, dhidi ya Dodoma Jiji FC.

Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri ulimalizika kwa kwa matokeo ya sare ya bila kufungana.

Young Africans imerejea Dar es salaam kujiandaa na mchezo wa Fainali Kombe la Shirikisho dhidi Simba SC utakaopigwa mjini Kigoma Julai 25, Uwanja wa Lake Tanganyika.

Simba SC kuiwahi Young Africans Kigoma
Gridi ya taifa kuunganishwa kisiwa cha Maisome