Kikosi kimewasili salama uwanja wa ndege wa kimataifa wa Victor Attah, Uyo-Nigeria tayari kwa mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Robo Fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Young Africans itakuwa mgeni wa Rivers United Jumapili (April 23), katika Uwanja wa Godswill Akpabio.

Kikosi Cha Young Africans kimewasili Uwanja wa ndege wa Victor Attah mchana huu kwa saa za Afrika mashariki kikitokea Uwanja wa kimataifa Murtala Muhammed, mjini Lagos.

Beki wa kati wa Klabu hiyo,Mamadou Doumbia ni Miongoni mwa Wachezaji waliopo kwenye msafara huo Baada ya kurudi kutoka Nchini Mali alikoenda kwenye mazishi ya Baba yake mzazi.

Bukoba: Mudir JASUTA ahimiza waumini utoaji zaka
Inzaghi: Ni kama ndoto kucheza nusu fainali