Mshambuliaji Pierre Emerick Aubameyang amepata mchongo wa kuachana na nyakati ngumu za Chelsea baada ya kusajiliwa na klabu ya Ligue 1, Olympique Marseille.

Aubameyang amekuwa na wakati mgumu huko Stamford Bridge tangu aliponaswa kwa Pauni 10 milioni akitokea FC Barcelona, Septemba mwaka jana, akifunga mabao matatu tu katika mechi 21.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Gabon, aliwekwa kando pia na Chelsea kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu uliopita baada ya The Blues kuwa na wachezaji wengi walionaswa kwenye dirisha la Januari mwaka huu.

Baada ya kushindwa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Chelsea na makocha watatu tofauti, Aubameyang anatarajia kuachana na Chelsea baada ya ujio wa kocha Mauricio Pochettino.

Awali, Auba mwenye umri wa miaka 34, alitajwa kuwa na mpango wa kwenda Saudi Arabia, lakini sasa amekubali kwenda Marseille kwa dili la miaka miwili na mwaka watatu wa ziada.

Marseille imekamilisha mazungumzo na Chelsea kukamilisha dili la kumnasa Mshambuliaji huyo, ambaye mkataba wake huko Stamford Bridge ulikuwa umebakiza mwaka mmoja, akiwa analipwa Pauni 160,000 kwa juma.

Pochettino kwenye kikosi chake ameshanasa Washambuliaji wakutosha wakiwamo Christopher Nkunku, Andrey Santos, Malo Gusto na Nicolas Jackson.

Ihefu FC wamtia pini Victor Akpan
Mwinyi Zahera aanza makeke Coastal Union