Msanii wa Maigizo na Mchekeshaji , Peter Mollel maarufu kama ‘Pierre Liquid’ amethibitisha kuwa amepata maambukizi ya virusi vya Covid 19 (corona).

Akizungumza kwa njia ya simu na gazeti la Mwanaspoti Pierre amesema kwa sasa yupo hospitali ya Amana akiwa anaendelea kupatiwa matibabu.

Amesema aliamua kwenda kupima hospitali ya Temeke baada ya boss wake wa karibu kugundulika kuwa ameathirika na ungonjwa huo.

“Nina bosi wangu wa karibu ambaye kapata ugonjwa huu na kwa kuwa mara nyingi tuko naye alinishauri na mimi nikapime kwa nia njema ili kama ninao nipate matibabu mapema na kuepuka kuwaambukiza wengine. ” Amesema Piere

Na kuongeza kuwa, hivyo nilienda hospitali ya Temeke, wakanipima ndipo nilipokutwa ninao na kuletwa hapa Amana ambapo kwa sasa ni moja ya kituo cha wagonjwa,”

Alipoulizwa anadhani ni wapi kaupatia, amesema “Huu ugonjwa mimi nitakuwa nimembukizwa nikiwa baa hakuna sehemu nyingine kwa kuwa ndio maeneo yangu ya kujidai,”.

Wachezaji Chelsea wakubali
TANZIA: Mchungaji Rwakatare afariki dunia, mwanaye aeleza chanzo