Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda amewashukia watu wanaodaiwa kuwa wanataka kuwania nafasi ya kugombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 2020.
Akizungumza jana jijini Dodoma katika uzinduzi wa mradi wa vibanda vya biashara vya chama hicho, Pinda alieleza kuwa wanaofanya mchakato huo wanajisumbua na kutapatapa kwani sio utamaduni wa chama.
Kada huyo mwandamizi wa CCM alisema amekuwa akisikia kuna mtu anayetapatapa kuusaka urais 2020 akilenga kumpinga Rais John Magufuli. Alisema kwa jinsi alivyofanya kazi na Serikali za awamu zote nne, anajua jambo hilo haliwezekani.
Aidha, alifafanua kuwa Rais Magufuli anaelekea kumaliza awamu yake ya kwanza na ataendelea na awamu yake ya pili na sio vinginevyo, huku akidai huenda kukawa na minong’ono baada ya awamu ya pili kumtaka aongezewe muda.
Katika kipindi cha hivi karibuni, kumekuwa na mvutano kati ya baadhi ya makada wa chama hicho huku kukiwa na tetesi za aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nchi, Bernard Membe kutaka kuwania nafasi ya kugombea urais 2020.
-
Raia wa tano wakigeni wanaohusishwa kumteka Mo Dewji kukamatwa
-
Kamanda Muroto awatahadharisha matapeli jijini Dodoma