Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda, jana alirudisha fomu za kuwania nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi baada ya kuzunguka mikoa ya Tanzania na kufanikiwa kupata idadi ya wadhamini waliohitajika.

Pinda alirejesha fomu hizo kwenye ofisi kuu ya chama hicho mjini Dodoma na kumkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajab Luhavi.

Baada ya kurejesha fomu hizo, mtoto wa mkulima ambaye aliambatana na familia yake aliwaambia waandishi wa habari kuwa hataugua moyo endapo chama chake hakitapitisha jina lake kwa kuwa ni Mungu pekee amjuaye rais ajaye.
unnamed (11)

Makada wa Chama hicho wenye nia ya kugombea nafasi ya urais wameendelea kurudisha fomu ikiwa kesho (July 2, 2015) itakuwa siku ya mwisho kwa watangaza nia wote kurejesha fomu ili kupisha hatua nyingine za kumpata mgombea mmoja.

Argentina Kiboko, Yaifuata Chile Fainali Kwa Kipigo Kitakatifu
Mafuta Bei Juu, Walioyaficha Kuanza Kuadhibiwa