Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Godfrey Pinda, amewataka watanzania wawe na utulivu wakati ambao muda unatakiwa kwa ajili ya kuipitia katiba na kuangalia maeneo yaliyo na tatizo ili yarekebishwe.

Pinda ameyasema hayo jana wakti akizindua magari mawili ya Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora yaliyokabidhiwa kwao kwa ajili ya kutekeleza kazi na majukumu mbalimbali katika maeneo tofauti nchini.

Pinda amesema katiba ya sasa haina tatizo lolote ila wanaoitafsiri ndio wanaotoa maana tofauti na kunyanyua hisia mchanganyiko kwa jamii.

Amesema katiba ni kama kitabu cha dini ambapo kila anaesoma hujitokeza na maana tofauti jambo ambalo linaleta mkanganyiko kwa jamii inayosikia uchambuzi usio na ukweli na kuamini kabla ya kuisoma.

“Kama katiba ya sasa ingekua na tatizo basi hata serikali na uongozi wake isingeweza kutekeleza miradi yake na kusimamia maendeleo ya nchi ipasavyo,” amesema Pinda.

Pinda amezitaka Taasisi zinazopata nafasi ya kujadili katiba ziweze kutoa elimu sahihi kwa jamii ili waweze kuielewa katiba nzima na sio kutembea na vipengele vichache kama mfano na kuipotosha jamii.

Bluce Willis kutoonekana tena kwenye filamu
Rais Samia aagiza MSD kufumuliwa