Ni dhahir FC Barcelona watawakosa wachezaji Gerard Pique na Sergi Roberto katika michezo kadhaa ijayo, kufuatia wawili hao kukabiliwa na majeraha.

Beki Pique aliumia goti mwishoni mwa juma lililopita akiwa kwenye mchezo dhidi ya Atletico Madrid, ambao ulimalizika kwa FC Barcelona kufungwa bao moja kwa sifuri.

Taarifa kutoka FC Barcelona zinaeleza kuwa, beki huyo mwenye umri wa miaka 33, atakuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi 5.

Kwa upande wa beki na kiungo Sergi Roberto aliumia misuli wakati wa mchezo dhidi ya Athletic Bilbao, na atakua nje kwa miezi 2.

Kuumia kwa wawili hao ni habari mbaya kwa meneja Ronard Koeman na mashabiki wa FC Barcelona, kutokana na msimu huu kuwa na mwenendo mbaya kwao.

Kupotezea mchezo dhidi ya Atletico Madrid, kunaifanya Barca ishike nafasi ya 10 kwenye msimamo wa Ligi ya Hispania (La Liga).

Iran yaapa ‘kuichapa’ Israel ikifanya haya mwaka huu
Namungo FC wamkuna kocha Morocco

Comments

comments