Aliyekua mshambuliaji wa klabu ya Chelsea, Claudio Pizarro amerejea tena nchini Ujerumani na kujiunga na klabu ya Werder Bremen.

Pizarro amerejea kwenye klabu hiyo ambayo aliwahi kuitumikia kwa vipindi vitatu tofauti na kupokelewa kwa shangwe na mashabiki ambao walijitokeza uwanja wa ndege kumlaki wakati akiwasili.

Kusudio kubwa ambalo lilikua chagizo kwa viongozi wa Werder Bremen kumsajili mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 36, ni kuwa huru baada ya kuachwa na klabu ya FC Bayern Munich mwishoni mwa msimu uliopita.

Tayari klabu za mashariki ya kati (Uarabuni) zilikua zimeshaonyesha nia ya kutaka kumsajili Pizarro, lakini uwepo wa klabu hiyo ya nchini Ujerumani ulivuruga mipango hiyo.

Kwa mara ya kwanza Pizarro aliitumikia Werder Bremen kuanzia mwaka 1999–2001 na baada ya hapo aliondoka na kujiunga na FC Bayern Munich kati ya mwaka 2001–2007 kabla hajaelekea nchini England kujiunga na Chelsea kuanzia mwaka 2007–2009.

Baada ya mambo kuwa magumu akiwa na The Blues, Pizarro alirejeshwa nchini Ujerumani na kujiunga na Werder Bremen kwa mkopo mwaka 2008 na baada ya hapo alisajiliwa moja kwa moja kuanzia mwaka 2009 hadi 2012.

Inler: Tukitanguliza Furaha Ya Kufuzu Itakula Kwetu
Idadi ya Waliofariki Kwenye Mkutano Wa Magufuli Yaongezeka