Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA, Michel Platini, anatarajia kutangaza kuwania nafasi ya urais wa shirikisho la soka duniani FIFA siku kadhaa zijazo.

Platini, alitoa ahadi ya kufanya hivyo baada ya kutafuta ushauri miongoni mwa wajumbe wa kamati ya utendaji ya UEFA, ambayo kwa asilimia kubwa wanahitaji kumuona kiongozi huyo wa soka barani Ulaya akiiongoza FIFA.

Raia huyo wa nchini Ufaransa, alitarajiwa huenda angewani nafasi ya urais wa FIFA katika uchaguzi uliofanyika mwanzoni mwa mwezi May, lakini hakufanya hivyo kwa kisingizio cha kuheshimu maslahi ya UEFA.

Hata hivyo Platini, alionekana kuwa sambamba na baadhi ya wadau wa soka duniani ambao walimtaka rais wa sasa wa FIFA Sepp Blatter, kuachia madaraka mara baada ya kuibuka kwa kashfa ya ulaji wa rushwa, kitendo ambacho kiliendelea kuonyesha alikua hakubaliani na uongozi wa mzee huyo kutoka nchini Uswiz.

FIFA wanatarajia kufanya uchaguzi wa rais mwanzoni mwa mwaka ujao (Februari 26), kufuatia Sepp Blatter kutangaza kujiuzulu miezi miwiwli iliyopita kutokana na sakata la uchafu wa rushwa ambalo linawakabili maafisa wa FIFA baada ya kufanyiwa uchunguzi na shirika la upelelezi la nchini Marekani FBI.

Hamad Rashid Aahidi Kujisalimisha Jela
Diaby Aikacha West Bromwich Albion