Kiungo kutoka nchini Ufaransa Paaul Pogba, bado yupo kwenye hali ya ‘SINTOFAHAMU’ kuhusu kusaini mkataba mpya na Uongozi wa Klabu ya Manchester United.

Pogba amekua katika hali ya kusubiri kwa majuma kadhaa, huku akiwataka viongozi wa klabu hiyo kumpa muda, na jibu kubwa analolitoa kila mara husema “ngoja tusubiri tuone nini kitatokea baadae.”

Hali hiyo inaendelea kutoa mwanya kwa wadau wa soka duniani kuhisi huenda kiungo huyo akaikacha Manchester United mwishoni mwa msimu huu, kufuatia kuhusishwa na mpango wa kuwaniwa na klabu za Juventus na Real Madrid.

Taarifa za hivi karibuni zilibainisha kwamba, huwenda Pogba akaongeza mkataba mpya na mashetani wekundu, kufuatia mkataba wa sasa kutarajiwa kufikia kikomo mwishoni mwa msimu huu.

Ripoti hiyo imesema kwamba, kusajiliwa kwa Cristiano Ronaldo na Jadon Sancho kumemfanya Pogba ashawishike kubakia klabu hapo, lakini bado hajafanya maamuzi ya kusaini mkataba mpya.

Hata hivyo, akizungumza baada ya ushindi dhidi ya Ubelgiji, Pogba aliiambia Sport Mediaset: “Mara zote huwa nazungumza na wachezaji wenzangu wa zamani kama Paulo (Dybala).

“Mimi bado nipo Manchester United, nina mwaka mmoja kwenye mkataba wangu wa sasa na tunaona nini kitakachojiri.

“Nataka kumaliza msimu vizuri hapa, halafu tutaangalia nini kitakachotokea baadae.”

Matajiri wa Newcastle United waunguruma
Gomes azinasa mbinu za Jwaneng Galaxy