Kiungo kutoka nchini Ufaransa Paul Pogba amepasua ukweli wa mambo baada ya usajili wake kukwama wakati wa majira ya kiangazi kabla ya kufungwa mwishoni mwa mwezi uliopita.

Pogba, ambaye aliwaniwa na klabu za Chelsea, Man Utd, Man City, Real Madrid pamoja na FC Barcelona, amesema alikua chanzo cha dili lake kufeli kutokana na maamuzi aliyoyachukua dakika za mwisho.

Pogba, amelazimika kusema ukweli wa jambo hilo, baada ya mtendaji mkuu wa klabu ya Juventus, Giuseppe Marotta kueleza kinaga ubaga kilichopelekea mambo kuwa magumu huku akiitaja Chelsea ilikaribia kumsajili mchezaji huyo.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 22, amesema alijifikiria mara mbili na kuona hakuan haja ya kuachana na Juventus katika kipindi hiki kutokana na kuamini kwamba muda wake wa kundoka klabuni hapo bado haujafikia.

Amesema amekua na maisha mazuri ndani ya klabu hiyo inayotetea taji nchini Italia, na pia alizingatia umri alionao na kubaini bado ana nafasi ya kuendelea kutamba barani Ulaya.

Hata hivyo Pogba amesisitiza ipo siku huenda akaondoka klabuni hapo na kusaka mahala pengine pa kucheza soka lake kutokana na mazingira ya soka yanavyoendelea kubadilika siku hadi siku.

Chelsea, walitajwa huenda wangefanikiwa kumsajili Pogba baada ya kusalia kwenye harakati za uhamisho wa mchezaji huyo, lakini walikwamishwa na ada kubwa ya paund million 62 ambazo ni sawa Euro million 85 ambazo zilikua zikihitajika huko Juventus Stadium.

Kocha Wa England Afichua Siri Za Arsenal
Mgosi: Stars Inahitaji Kumaliza Kiu Ya Wabongo