Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenenzi, Humphrey Polepole amefunguka na kuhoji kuhusu kitendo cha Chadema kumficha dereva aliyeshuhudia tukio zima la shambulio la risasi kwa mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na amewataka wananchi wa jimbo la Siha kumhoji Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aeleze sababu za kufanya hivyo.
Ametaka kuhoji siri iliyopo inayowafanya Chadema wamfiche dereva huyo wakati anahitajika kuisaidia Serikali kufumbua ukweli na kumjua aliyehusika katika shambulio hilo.
-
Video: Polepole avunja ukimya Lissu kupigwa risasi, Rafu za uchaguzi zaanza Kinondoni
-
Mtaa wateketea kwa moto jijini Nairobi
Amesema viongozi wa vyama vya upinzani wamekuwa wakitengeneza chuki na ugomvi baina ya wananchi na Serikali na kusema siasa hizo zimepitwa na wakati na kuwataka wananchi kuwadharau.
Polepole ameeleza kuwa katika tukio hilo la Lissu kupigwa risasi mtu ambaye angelielezea vizuri ni dereva ambaye alikuwa akimuendesha Lissu.
”Natambua kuwa tukiwa katika kampeni zinazoendelea Mbowe yupo katika jimbo hili akiendesha siasa za uchochezi baina ya Serikali na watu wake, sasa naomba mumhoji ni kwa nini mpaka sas hawataki kumtoa dereva wa Lissu walipomficha ili aeleze ukweli kuhusu tukio hilo kama hakuna siri ndani yake wanayoificha ” amesema Polepole.
Polepole ametoa kauli hiyo jana wakati wa kampeni ya kumnadi mgombea ubunge wa Siha, DK.Godwin Mollel uliofanyika katika kijiji cha Sinai, kata ya Ormelili.