Chama Cha Mapinduzi (CCM), kupitia Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi, Humphrey Poleplole kimejibu ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ambayo hivi karibuni imewaibua wengi, Polepole ameagiza hatua kali kuchukuliwa dhidi ya watu wanaopotosha umma kufuatia ripoti hiyo ya CAG.
Polepole amezungumza hayo leo na waandishi wa habari ambapo amesema kuna watu wameacha kuzungumzia maendeleo wanaikosoa Serikali hata kama imefanya vizuri, ameomba Watanzania kudumisha uzalendo.
”Katika ripoti ya CAG kuna vyama vya siasa vimetumia mamilioni ya fedha halafu haohao ndio vihelehele wa kuikosoa Serikali. Ripoti inaonyesha Chadema wamekuwa wakipewa zaidi ya milioni 520, hawajioni ila wanaiona CCM. Hawa ndio wakuwachukulia hatua maana wanapotosha umma” amesema polepole.
Ameongezea ”Kuna mtu mmoja anaongoza kwa upotoshaji juu ya ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG. Chama chake kina mbunge mmoja tu wa ACT Wazalendo. Sijui kasoma shule gani huyu. Kaja anasoma juu juu tu eti trilioni 1.5. Ana bahati ndugu Magufuli ni mpole ila tushawambia mwaka 2020 akatafute kazi ya kufanya. Pia arudi shule akasome kwani hakuna shilingi moja iliyopotea, ameongezea Polepole”.
Polepole amezungumza hayo kufuatia ripoti ya CAG iliyotolewa na kuchambuliwa na Mbunge wa Kigoma Zitto Kabwe ikidaiwa kuwa kuna opotevu wa fedha kiasi cha trilioni 1.5 zilizodaiwa kukusanywa na Serikali lakini hazikutumika wala kukaguliwa.