Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Humphrey Polepole amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita Modest Alpolnary, kutenga kiasi cha Shilingi Milioni 200 kwa ajili ya vijana na wanawake.

Polepole amesema hayo wakati wa uzinduzi wa Geita ya Kijani ulioandaliwa na UVCCM Mkoani humo.

Amesema fedha hizo ni kwa ajili ya kuvisaidia vikundi vya vijana na Wanawake wa chama hicho kuanzisha viwanda.

”Wote wapigwe semina, waambiwe maana ya viwanda hivyo, waambiwe namna ya fursa zilizopo, wapewe ujuzi wa namna ya kuviendesha” amesema Polepole.

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Geita, Manjale Magambo amemuomba Polepole kufikisha kilio cha vijana ambao, wamekuwa wakifukuzwa kazi na  baadhi ya Migodi ya dhahabu hapa nchini na kisha taarifa zao kusambazwa kwenye migodi yote ili wasiajiliwe popote pale.

Walimu 10 mbaroni kwa wizi wa mitihani
Rais Ramaphosa kuukosa mkutano wa UN