Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amemponda kiongozi mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe kwa kuendesha vikao vikuu vya chama chake kupitia mitandao ya Kijamii.
‘’Siku hizi, hata vikao vya kamati kuu ya ACT-Wazalendo, Zitto amekuwa akivifanyia mtandaoni, na kuhoji inakuwaje kikao kikubwa kama hicho kinaandaliwa mtandaoni tena kupitia facebook” amesema Polepole.
Ameongezea ACT-Wazalendo kimekwisha kimebakia kwenye mitandao ya kijamii ukiwemo wa Facebook na kwamba hivi karibuni wanachama wake kutoka mikoa miwili waliomba kujiunga na CCM.
-
Washikiliwa na Polisi kwa kupiga ramli chonganishi
-
Siwezi kwenda mafichoni, nitarudi Tanzania- Lissu
‘’Ukweli nawaambia isingekuwa huruma ningekuwa nimeshawafagia wote, yaani wote, lakini tukasema tumuache angalau ana watu kadhaa ili chama kionekane kina uhalali wa kuendelea kuwa kwenye daftari la Msajili wa Vyama vya siasa’’amesema Polepole.
Polepole amezungumza hayo pindi akiwapokea wanachama wapya 360 wakiwemo waliohama vyama vya Chadema na ACT-Wazalendo na kujiunga CCM jijini Mbeya.
Aidha Polepole amewashukuru wanachama hao wapya kwa uamuzi waliouchukua kujiunga na Chama sahihi CCM.