Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, leo saa 10:00 jioni, atawaapisha wabunge wawili wa Bunge hilo walioteuliwa na Rais Dkt. John Magufuli, mapema jana.

Taarifa hiyo imetolewa hii leo Novemba 30, 2020, na ofisi ya Bunge, ambapo imeeleza kuwa wabunge watakaoapishwa ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Hamphrey Polepole, na aliyekuwa mbunge wa viti maalum katika Bunge la 11 kupitia chama cha CUF, Riziki Lulida.

Spika Ndugai anawaapisha wabunge hao kwa kuzingatia kanuni za kudumu za Bunge inayoeleza kuwa endapo mbunge atachaguliwa au kuteuliwa kipindi ambacho hakuna mkutano wa Bunge unaoendelea, Spika atamwapisha katika eneo atakalolipanga na atatoa taarifa kwenye kikao cha kwanza cha mkutano wa bunge utakaofuata.

Kiswahili kuanza kutumika katika shule Afrika Kusini
Simba SC kurudi kesho Jumanne

Comments

comments