Katibu wa Itikadi na Uenezi  wa  Chama Cha Mapinduzi CCM, Humphrey Polepole amemtahadharisha Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema kwakumwambia kuwa  kipindi hiki ni cha mwisho kuongoza Jimbo hilo la Arusha Mjini.

Hayo yamekuja mara baada ya Mbunge huyo kupitia kurasa zake za twitter kujibizana huku Lema akionyesha kumhoji Polepole kama familia yake huwa inamuelewa kweli anachokizungumza.

“Term ya mwisho Arusha, tunataka Mbunge wa Masuala na si wa Matukio, hata mkichezesha draft ili uende Hai, haitawezekana maana hata “fly to…” maji yako shingoni, na ukiamua kurudia kazi yako ya zamani. anko Siro is very serious,”ameandika Polepole

 

Lissu: Bunge halijatoa hata senti moja
Kangi Lugola apata pigo