Mahakama nchini Kenya imemfutia dhamana askari wa jeshi la polisi anayekabiliwa na mashtaka ya kumbaka mkimbizi mwenye umri wa miaka 40.
Askari huyo aliyetambulishwa kama constable Kennedy, anadaiwa kufanya tukio hilo la ubakaji mwaka 2019, katika Kaunti ya Trukana, eneo la Kakuma 4 Patrol.
Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Lodwar, Mwangi K Mwangi alizuia dhamana ya mtuhumiwa huyo akieleza kuwa alipotea baada ya kupata thamana hiyo mwaka 2019.
Taarifa zilizowasilishwa mahakamani hapo zilieleza kuwa mtuhumiwa alikamatwa tena na kitengo maalum cha polisi, baada ya kumtafuta kwa miaka miwili.
Upande wa mashtaka umeandaa mashahidi 13 katika kesi hiyo, ambapo inatarajiwa kuanza kusikilizwa Septemba 2, 2021.