Askari Polisi nchini wametakiwa kuchangamkia fursa ya kujiendeleza kitaaluma inayotolewa na Jeshi la Polisi ndani na nje ya nchi, kwa kushirikiana na vyuo mbalimbali vinavyotoa elimu ya juu ili kuendana na maboresho ya mifumo ya kisasa ya TEHAMA, iliyopo katika utendaji wa Jeshi la Polisi.
Rai hiyo imetolewa na Kamishna wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali watu wa Jeshi la Polisi, CP Suzan Kaganda wakati akikagua mfumo wa kielektroniki wa haki jinai katika kituo cha Polisi Bukoba.
Aidha, amewataka viongozi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera kusimamia utendaji wa Jeshi la Polisi kwa kuzingatia haki, nidhamu na weledi.
CP Kaganda pia amewataka Askari kushiriki kwenye michezo, ili kuimarisha afya zao kimwili na kiakili kwa ajili ya kuwahudumia Wananchi kwa weledi.