Jeshi la Polisi jijini Dar es salaam limeanza msako mkali kuwatafuta watu waliohusika na mauaji ya Mkurugenzi na Mwanzilishi-Mwenza wa Shirika lisilokuwa la kiserikali la PAMS Foundation, Wayne Lotter.

Lotter aliuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana maeneo ya Masaki alipokuwa akitokea uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu Julius Nyerere (JNIA)

Aidha, mwanaharakati huyo ndiye aliyefanikisha kukamatwa kwa mfanyabiashara, Yang Feng Glan maarufu kama jina la ‘Malkia wa Meno ya Tembo’ hivi karibuni baada ya mhalifu huyo kusakwa kwa muda mrefu katika mataifa mbalimbali duniani.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe amesema kuwa amesikitishwa sana na mauaji hayo kutokea kwa mwanaharakati huyo kwani alikuwa ni msaada mkubwa katika kupiga vita ujangili.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema kuwa linaendelea na msako mkali wa kuweza kuwabaini wahusika wote wa mauaji ya mwanaharakati huyo wa kupinga ujangili.

 

Ummy Mwalimu aagiza kuboreshwa kwa huduma za afya
Makonda kuendesha kampeni kujenga nyumba 402 za walimu Dar