Jeshi la Polisi jijini Dar es salaam limesambaratisha mkutano wa Sheikh Issa Ponda ambao ulikuwa unatakiwa kufanyika katika hoteli ya Iris, Kariakoo jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa amepanga kuzungumzia sakata la Tundu Lissu kupigwa risasi.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa kamati ya uongozi ya CUF, Julius Mtatiro ambapo amesema kuwa polisi wamezuia mkutano huo huku baadhi ya waandishi wa habari waliokuwepo kwenye ukumbi huo wakikamatwa.

“Polisi wamevamia mkutano wa Sheikh Issa Ponda katika hoteli ya Iris, Kariakoo. Taarifa za awali zinasema baadhi ya waandishi wamekamatwa. Sheikh Ponda alikuwa azungumze na vyombo vya habari kuhusu suala la Kupigwa risasi kwa Tundulissu asubuhi hii, mara baada ya kurejea kutoka Nairobi ambako alizungumza na Lissu,”amesema Mtatiro

 

 

Baada ya kufuzu kombe la dunia Panama yatangaza siku kuu
Mataifa 22 yapata tiketi ya kombe la dunia 2018