Watu 6 wakiwemo Raia wa Burundi na wafuasi wa kikundi cha waasi cha FDD NDD cha nchini humo, wameuawa wakati wakitekeleza tukio la ujambazi jijini Dar es salaam ambapo silaha za kivita na risasi zimekamatwa.

Hayo yamesemwa na Kamishna wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamanda Lazaro Mambosasa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema kuwa Jeshi hilo limefanikiwa kumkamata jambazi sugu ambaye amewahi kutekeleza matukio mengi ya uhalifu na kuua raia kadhaa wakiwemo Polisi katika mikoa mbalimbali nchini.

“Watuhumiwa hao walikamatwa baada ya kuwepo kwa matukio ya uhalifu yaliyotokea huko Mabibo External, ambapo mfanyabiashara wa TIGOPESA/MPESA aliporwa shilingi milioni 50 na huko Tegeta mfanyabiashara raia wa China ambaye aliporwa shilingi milioni 10,” amesema Kamanda Mambosasa.

Hata hivyo, ameongeza kuwa matukio mengine waliyoshiriki ni pamoja na kuteka mgodi wa Tulawaka Geita mwaka 2011, kuvamia maduka ya kubadilishia fedha za kigeni huko Zanzibar, mwaka 2012 walivamia kituo cha mafuta mkoani Kagera na kufanya mauaji, Pia walivamia maduka yaliyopo karibu na kituo cha Polisi Chato na hivyo kukishambulia kituo ili kurahisisha uporaji.

 

Mhagama atoa maagizo kuhusu miundo mbinu ya jiji la Dar
Basi la Rungwe Express lapata ajali mbaya mkoani Morogoro