Jeshi la polisi Mkoani Dodoma limejipanga vizuri kukabiliana na wale wote watakaohatarisha amani wakati na baada ya uchaguzi mkuu.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo Agosti 27, 2020 jijini Dodoma Kamanda wa polisi  mkoani humo Gilles Muroto amesema kuwa makundi yote ambayo yamejiandaa kwa ajili ya  kuleta vurugu yatashughulikiwa.

“Jeshi la polisi kazi yake ni kuhakikisha kuna amani, hakutakuwepo na makundi ya Ovyo,Tanzania huwa naifananisha na mto wa maji mtulivu,mto wa maji mtulivu mara nyingi kuna kuwa na miti mikubwa ya maua  mazuri imeizunguka ule mto” amesema Kamanda Muroto.

Kamanda Muroto ameongeza kuwa jeshi la Polisi litahakikisha linafuatilia kwa makini mwenendo wa kampeni.

TCU yafungua dirisha 2020/21

Katika hatua nyingine, Kamanda Muroto ametoa wito kwa watanzania kuacha watu wa kulinda nyumba pindi wanapokwenda kwenye shughuli mbalimbali ili pasitokee uhalifu wowote.

KUMEKUCHA: Messi atunisha msuli Barcelona
Wakulima Mkonge wajazwa pesa