Haruna Juma – Katavi.

Jeshi la Polisi Mkoani Katavi, limefanikiwa kuwakamata watu 13 na Pikipiki ya magurudumu matatu ‘Bajaji’ aina ya TVS yenye namba MC643-DCE wanayotuhumiwa kuitumia kutekeleza uhalifu ikiwemo mauaji.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi ACP, Kaster Ngonyani amewaambia Wanahabari kuwa bajaji hiyo ilikuwa inatumiwa na wahalifu kuwatoa sehemu moja kwenda nyingine kutekeleza mauaji na kukimbia.

Mbali na Bajaji hiyo, ACP Ngonyani amesema Jeshi la polisi Mkoani Katavi linawashikilia watuhumiwa hao 13 waliokuwa wanajihusisha na mauaji hayo.

Ameongeza kuwa, katika kipindi cha mwezi Oktoba 2023 pekee jumla ya watuhumiwa 196 wamekamatwa na Jeshi la Polisi wakihusishwa na matukio mbalimbali.

CORECU yawapa siri Wakulima wa Korosho Pwani
Wakaguzi zingatieni weledi kazini - ACP Katabazi