Polisi wa Zimbabwe wanachunguza shambulio dhidi ya waandishi wa Habari akiwemo Annahstacia Ndlovu ambaye anasema yeye na waandishi wengine walipigwa na kunyanyaswa na wafuasi wa chama tawala cha Zanu-PF katika jiji la Bulawayo.

Kufuatia hatua hiyo, Chama cha Waandishi wa Habari nchini Zimbabwe kimekusanya taarifa za kunyanyaswa au kushambuliwa kwa waandishi na wafuasi wa chama Tawala, ikiwemo kunyimwa fursa ya kushiriki mikutano ya kampeni.

Maelezo ya waandishi wa waandishi wa Habari kunyanyaswa, kushambuliwa au kunyimwa haki ya kuripoti uchaguzi Mkuu wa Zimbabwe, yanadaiwa kuleta wasiwasi kwa wachambuzi wa vyombo mbalimbali vya Habari.

Katibu Mkuu wa Muungano wa Waandishi wa Habari wa Zimbabwe, Perfect Hlongwane anasema watashirikiana na Polisi na vyama vya siasa kujaribu kuboresha uhusiano na Vyombo vya Habari kabla ya uchaguzi mkuu.

Hatma ya Mcameroon mikononi mwa Minziro
Kramo: Nitapambana hadi kieleweke