Abel Paul, Jeshi la Polisi – Tanga.
Jeshi la Polisi nchini, limesema litaendelea kushirikisha Jamii katika kupambana na uhalifu katika maeneo mbalimbali Nchini, huku likipongeza wadau wenye mapenzi mema na Jeshi hilo kwa ushirikiano wanaouonesha katika mapambano dhidi ya uhalifu.
Hayo yamesemwa leo Agosti 10, 2023 Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga na Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam – DPA, Kamishna Msaidizii Mwandamizi wa Polisi, SACP- Dkt. Lazaro Mambosasa wakati alipotembelea viwanja vya mafunzo na mbinu za Medani za kivita, eneo la Mkomazi.
SACP Mambosasa, pia amewapongeza Islamic Help kwa mafano mzuri waliouonesha wakuchimba kisima katika viwanja hivyo na kuwaomba wananchi kuendelea kuiga mfano huo mzuri.
Kwa upande wake Balozi wa Maji kutoka Tanga, Habibu Mbota amesema wanaendelea na uchimbaji wa kisima hicho na wamehadi siku chache zijazo watayafikia maji ambayo yatatumiwa na Askari wa kozi ya Uofisa na Mkaguzi Msaidizi ambao ni zaidi ya elfu moja waliopo kambi hiyo ya mafunzo ya medani za kivita Mkomazi.
Akilishukuru Jeshi la Polisi, mkazi wa Mkomazi Rashid Juma amesema uwepo wa Jeshi la Polisi katika eneo la Mkundi mbaro Mkomazi unahitaji huduma za kijamii ikiwemo Maji, na kuchimbwa kwa kisima hicho kitakuwa msaada mkubwa kwao.