Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amesema Vikosi vya usalama vitawasaka waliohusika na vifo vya muongoza Watalii na Watalii wawili wa kigeni, waliokuwa wakienda fungate katika mbuga ya Wanyama.

Museveni amelishutumu kundi la Allied Democratic Forces – ADF, kwa kuwaua wanandoa hao, raia wa Afrika Kusini na raia wa Uingereza, na muongoza Watalii wa Uganda siku ya Jumanne jioni Oktoba 17, 2023 karibu na Mbuga ya Kitaifa ya Queen Elizabeth.

Yoweri Museveni

Kundi hilo la ADF, ambalo lilianza kama la uasi nchini Uganda baadaye liliweka makao yake katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo – DRC, tangu mwishoni mwa miaka ya 1990, likiahidi utiifu kwa kundi jingine la kigaidi la Islamic State.

Serikali iweke Vituo usambazaji Nishati ya Gesi - Kamati
Migogoro imeimarisha mahusiano - Putin