Jeshi la Polisi mkoani Geita, linawasaka watu zaidi ya 10 waliofanya uharibifu wa mali kwenye nyumba 3 tofauti za wagombea Udiwani na Ubunge jimbo la Chato kupitia CHADEMA.

tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Oktoba 13, 2020, ambapo walikuwa wanatarajia kumpokea mgombea Urais wa chama hicho, Tundu Lissu.

Kamanda wa polisi mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe, amesema mali zilizoharibiwa kuwa ni pamoja na bajaji mbili kuchomwa moto, kuvunjwa kwa vioo vya madirisha baada ya kupondwa mawe, pamoja na kubomoa madirisha mawili ya nyumba.

katika hatua nyingine Kamanda huyo amewasisitiza wagombea wa nafasi mbalimbali  za uongozi, kuzingatia muda wa kufanya kampeni ili kuepusha vurugu zinazotokea baada ya muda uliowekwa na Tume kuisha.

Kaze kutua Dar usiku mnene
Azam FC: Tupo kamili kuikabili Mwadui FC