Wazazi na walezi 23 Wilayani Newala, Mtwara wamekamatwa na kufikishwa Mahakamani kwa madai ya kushindwa kuwapeleka watoto wao kujiunga na masomo ya Kidato cha Kwanza 2020.

Kamata kamata hiyo ni kufuatia kutoridhishwa na mahudhurio ya wanafunzi wa kidato cha kwanza kupitia taarifa ya Elimu mkoani humo.

Hatua hiyo ni kufuatia agizo la Mkuu wa Mkoa Mtwara, Gelasius Byakanwa  alilolitoa hivi karibuni kwa watendaji wa kata, tarafa na vijiji la kuwakamata wazazi na walezi wote walioshindwa kuwapeleka watoto wao shule kujiunga na kidato cha kwanza mwaka wa masomo 2020.

”Sasa nimekuwa nikihamasisha watoto waende shule na wazazi mmekuwa mkikahidi kuwapeleka watoto shule, sasa hawa watakuwa mfano, OCD washa gari hili tuwape lifti hadi kituoni wazazi hawa kwa kutowapeleka watoto wao shule” amesema

Aidha, ameagiza kuwa wazazi hao wapigwe faini na watoe maelezo ya kwa nini wamekaidi agizo la mkuu wa mkoa la kuwapeleka watoto hao shule.

Hata hivyo siku 4 zilizopita wazazi 50, Wilayani Tunduru mkoa wa Ruvuma wamekamatwa na Jeshi la Polisi Wilayani kwa kosa la kutowapeleka shuleni watoto wao waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza.

Naye mkuu wa mkoa Arusha, Mrisho Gamba ametangaza kuwachukulia hatua za kuwasweka rumande wazazi wote ambao bado hawajawapeleka watoto wao kujiunga na kidato cha kwanza am,etoa tahadhari hiyo na kuwataka wazazi m ara moja kuwapelwka watoto wao shuleni.

RC Gambo amesema kuwa licha ya Mkoa huo kufaulisha Jumla ya watoto 35,254, lakini taarifa ya Januari 24, 2020, imeonesha kuwa ni wanafunzi 25,483, ambao ni sawa na asilimia 72 ndio wamewasili katika shule walizopangiwa.

“Kuanzia sasa wanafunzi kokote waliko, wazazi kokote waliko, viongozi wangu wote katika ngazi zote, wataanza msako maalumu wa kuwatafuta wazazi wote ambao watoto wao hawajapelekwa shule na tukimkamata mzazi tutamuweka lock up na dhamana yake ni mtoto kuripoti shuleni” amesema Gambo.

Waziri Mkuu atoa agizo kwa wazazi wenye watoto wanaosoma China
Fundi simu wasiosajiliwa mwisho Julai, TCRA yatangaza kibano