Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara limekuja na mbinu ya kufanya doria katika njia kuu usiku na mchana, ili kuzuia ajali na kuwakamata madereva wanaovunja Sheria za usalama Barabarani hasa nyakati za usiku.
Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Kamishna Msaidizi wa Polisi, George Katabazi wakati akipokea Gari aina ya Pro Box PT 1486 lenye thamani ya zaidi ya Shilingi 19 Milioni, lililotolewa na Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Manyara.
Akikabidhi gari hilo, Kaimu mwenyekiti wa Kamati, John Methew amesema litasaidia kufanya doria barabarani na kuzuia ajali hasa katika maeneo korofi kama kona za Kolo na milima ya Logia.
Awali, Mkuu wa Kikosi Cha Usalama Barabarani, Mrakibu wa Polisi Fredric Mpolo akiwataka Askari wa kikosi hicho kuongeza Kasi ya kutoa elimu kwa madereva na watumiaji wa barabara, ili kuzuia ajali.